Benin yatafuta kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati yake na China

(CRI Online) Machi 14, 2025

Rais wa Benin Patrice Talon amesema nchi yake iko tayari kufanya juhudi za pamoja na China ili kuendeleza maendeleo endelevu ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kunufaisha watu wa pande hizo mbili kutokana na matokeo ya ushirikiano wa kivitendo.

Rais Talon ametoa kauli hiyo wakati akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa China nchini humo Bw. Zhang Wei.

Ameongeza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya pande hizo mbili umedumisha kiwango cha juu, huku ushirikiano wa kunufaishana ukiendelezwa na urafiki wa jadi ukiimarishwa.

Kwa upande wake, Balozi Zhang We amesisitiza kuwa China inaweka mkazo mkubwa katika maendeleo ya uhusiano kati yake na Benin, pia inapenda kushirikiana na Benin kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili na matokeo yaliyopatikana katika Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Beijing, ili kuhimiza uhusiano wa washirika wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili katika ngazi mpya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha