Angola yasema serikali ya DRC na Kundi la M23 zinatarajia kufanya mazungumzo ya amani

(CRI Online) Machi 14, 2025

Ikulu ya Angola imesema, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 wataanza mazungumzo ya moja kwa moja ya amani huko Luanda, mji mkuu wa Angola, tarehe 18 mwezi huu.

Jumatano wiki hii, Msemaji wa Ikulu ya Rais wa DRC Tina Salama alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema, wamepokea mwaliko kutoka Angola, ingawa hakuthibitisha kama watashiriki katika mazungumzo hayo ya amani.

Kwa sasa, kundi hilo la M23 pia halijathibitisha kushiriki katika mazungumzo hayo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha