SADC kuondoa vikosi vyake DRC

(CRI Online) Machi 14, 2025

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imetangaza Jumanne wiki hii kwamba itasitisha jukumu lake la kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati ambapo mashambulizi yanayofanywa na kundi la waasi wa M23 yakizidi kuendelea.

Kwenye mkutano maalum uliohudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama, SADC iliamua kumaliza jukumu la Tume yake nchini DRC (SAMIDRC) na kuagiza vikosi hivyo kuondoka kwa awamu, uamuzi unaoashiria kubadilika kwa mtazamo wa SADC kuhusu mgogoro huo unaoendelea nchini DRC.

Mkutano huo umefanyika wakati mvutano mkali ukiendelea, ambapo waasi wa kundi la M23 wanakalia maeneo mengi katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha