China yatangaza mpango juu ya jitihada maalum za kuongeza matumizi katika manunuzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2025

BEIJING - China imetangaza mpango juu ya jitihada maalum za kuongeza matumizi katika manunuzi, wakati ambapo nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani ikielekea kufanya mahitaji ya ndani kuwa injini na nguzo kuu ya ukuaji wa uchumi.

Mpango huo uliotolewa jana Jumapili na Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Ofisi Kuu ya Baraza la Serikali la China, unalenga kuongeza matumizi kwenye manunuzi kwa nguvu kubwa, kuchochea mahitaji ya ndani katika sekta mbalimbali, na kuongeza uwezo wa matumizi kwa kuongeza mapato na kupunguza mizigo ya kifedha.

Pia unalenga kuzalisha ipasavyo mahitaji kupitia bidhaa zenye ubora wa juu, kuboresha mazingira ya matumizi katika manunuzi ili kuimarisha nia ya walaji kutumia fedha kwenye manunuzi, na kushughulikia vikwazo vinavyojitokeza kwenye matumizi.

Mpango huo, uliopangwa katika sehemu kuu nane, unatumia mbinu kamilifu kwa wakati mmoja kushughulikia mambo kama vile kukuza mapato, kuinua ubora wa matumizi kwenye huduma, kuboresha matumizi ya bidhaa kubwa na kuboresha mazingira ya matumizi katika manunuzi.

Mpango huo unalenga kuhimiza ukuaji mwafaka wa mishahara kwa kuimarisha uungaji mkono wa ajira ili kukabiliana na hali ya kiuchumi na kuboresha taratibu za marekebisho ya kima cha chini cha mshahara. Unasema kuwa, China itapanua njia za mapato ya kimali kupitia hatua za kutuliza soko la hisa na kuendeleza bidhaa nyingi za dhamana ambazo ni mwafaka kwa wawekezaji binafsi.

Mpango huo unatoa wito wa kuchunguza njia za kufungua thamani za nyumba zinazomilikiwa na wakulima kihalali kupitia mipango ya upangishaji, ushiriki wa usawa na miundo ya ushirika.

Hasa, mpango huo unasisitiza sekta zote za jadi za matumizi kama vile nyumba na magari, sambamba na kategoria zinazoibuka kama vile bidhaa wezeshwa na teknolojia za akili mnemba, uchumi wa anga ya chini na utalii wa watu wazima kuanzia umri wa miaka 50.

"China itaharakisha maendeleo na matumizi ya teknolojia na bidhaa mpya zikiwemo magari yanayojiendesha kiotomatiki, vitu vya kuvalika vyenye teknolojia ya akili bandia, video za ubora wa hali juu, miingiliano ya kompyuta na ubongo, roboti na utengenezaji wa kilaibu, unaojulikana zaidi kwa jina la uchapishaji wa 3D, ili kuunda sekta mpya za matumizi yenye ukuaji wa hali ya juu," mpango huo unasome.

Ipasavyo, China itafikiri kuanzisha mfumo wa ruzuku ya malezi ya watoto, kuongeza ruzuku ya fedha kwa ajili ya mafao ya kimsingi ya uzee na bima ya msingi ya matibabu kwa wakazi wa vijijini na wasiofanya kazi mijini, kufanya kazi kwa kutekeleza kwa umakini mfumo wa likizo ya mwaka yenye malipo -- kuhakikisha kwamba haki za wafanyakazi za kupumzika na likizo zinalindwa kisheria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha