Balozi wa Afrika Kusini nchini Marekani atakiwa kuondoka ndani ya saa 72

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2025

Picha hii iliyopigwa Oktoba 13, 2023 ikionyesha mwonekano wa mandhari yenye miti ya jacaranda mjini Pretoria, Afrika Kusini. (Xinhua/Zhang Yudong)

Picha hii iliyopigwa Oktoba 13, 2023 ikionyesha mwonekano wa mandhari yenye miti ya jacaranda mjini Pretoria, Afrika Kusini. (Xinhua/Zhang Yudong)

JOHANNESBURG - Ebrahim Rasool, Balozi wa Afrika Kusini aliyefukuzwa nchini Marekani, ametakiwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 72, ambapo Chrispin Phiri, msemaji wa Idara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini (DIRCO), amethibitisha kwa chombo cha habari nchini humo cha News24 juzi Jumamosi kwamba wamepokea uthibitisho rasmi kutoka kwa ujumbe wa Afrika Kusini nchini Marekani Ijumaa usiku kwamba Rasool amefukuzwa, na mipango imeshafanywa ya kurejea kwake.

Sanamu ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ikionekana mbele ya Majengo ya Muungano mjini Pretoria, Afrika Kusini, Desemba 5, 2023. (Xinhua/Zhang Yudong)

Sanamu ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ikionekana mbele ya Majengo ya Muungano mjini Pretoria, Afrika Kusini, Desemba 5, 2023. (Xinhua/Zhang Yudong)

Phiri amesema Rasool atazungumza na mamlaka za Afrika Kusini jijini Pretoria mara atakapokuwa amewasili Afrika Kusini. "Kutoka hapo, Pretoria itatathmini ni hatua zipi zitakazofuata zinazopaswa kuchukuliwa na kuzitekeleza," ameongeza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alimtangaza Rasool ni "mtu asiyekaribishwa" kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Ijumaa, kufuatia hotuba ya awali ya balozi huyo wa Afrika Kusini ambapo alimkosoa Rais wa Marekani Donald Trump.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi na Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, imeona kufukuzwa kimasikitiko kwa balozi huyo na na kuwataka wadau husika na walioathirika wote kudumisha hali ya kidiplomasia iliyoanzishwa katika kuwasiliana juu ya suala hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha