Barabara iliyojengwa na Kampuni ya China yachochea ukuaji wa kiuchumi na kijamii kaskazini mwa Namibia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2025

John Mutorwa (wa tano kushoto), naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Namibia, na wawakilishi kutoka China na Namibia, wakikata utepe kwenye ufunguzi rasmi wa Barabara ya John Mutorwa iliyojengwa na Kampuni ya China mjini Rundu, Namibia, Machi 14, 2025. (Picha na Musa Kaseke/Xinhua)

RUNDU, Namibia - Barabara ya John Mutorwa, iliyoko Rundu, katika Mkoa wa Kavango Mashariki kaskazini mwa Namibia, inasifiwa kuwa ni maendeleo makubwa ambayo yanaboresha muunganisho na kuchochea shughuli za kiuchumi katika jumuiya mbalimbali za wenyeji.

Barabara hiyo, iliyojengwa na Kundi la Kampuni za Ushirikiano wa Kimataifa la China Henan (CHICO), imefunguliwa rasmi siku ya Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita na kiongozi mwenye kubeba jina la barabara hiyo, John Mutorwa, naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Namibia, ikiashiria hatua muhimu kwa mkoa huo.

Mradi huo uliogharamiwa na serikali ya Namibia ulikamilika mwaka jana na tangu wakati huo umekuwa ukipongezwa kwa mchango wake wa haraka kwa wakazi na wafanyabiashara.

Jerry Kauyu, mdhibiti wa shehena katika Shirika la Masoko ya Kilimo na Biashara (AMTA), ambalo linahusika na usimamizi wa maeneo ya biashara ya mazao freshi, amezungumzia mchango wa barabara hiyo katika kuwezesha ufikiaji na kuunganisha jamii zilizokuwa zimetenganishwa hapo awali.

"Mimi ni mfanyakazi wa AMTA, mmoja wa wanufaika na barabara hii mpya iliyofunguliwa. Tumekuwa hapa tangu mwaka 2013, na barabara hii ni muhimu sana kwa sababu imeongeza safari zetu kwa watu wanaotembelea eneo la mazao freshi na jamii," amesema Kauyu katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua. "Kiukweli tunathamini maendeleo haya, na yanakuja wakati ambao yanahitajika sana kwa sekta hii yenye mazingira magumu."

Mbali na kuboresha usafiri, mradi huo pia umetoa fursa za ajira kwa wenyeji.

Akizungumza kwenye ufunguzi rasmi wa barabara hiyo, Mutorwa amebainisha kuwa wafanyakazi 61 wasio na ujuzi kutoka jamii za wenyeji waliajiriwa wakati wa awamu ya ujenzi, hii inaonyesha dhamira ya serikali ya kujenga barabara na kutoa fursa za kiuchumi kwa watu wake.

Cui Yunke, mkurugenzi mkuu wa CHICO nchini Namibia, ameliambia Xinhua kwamba ingawa mradi wa Barabara ya John Mutorwa ni wa kawaida kwa ukubwa, ni moja ya miradi "midogo na mizuri" ambayo imeleta manufaa halisi kwa jumuiya za wenyeji.

Wei Jinming, konsuli wa masuala ya kiuchumi na kibiashara wa Ubalozi wa China nchini Namibia, amebainisha kuwa kukamilika vizuri na kukabidhiwa kwa mafanikio kwa barabara hiyo ni mafanikio mengine katika ushirikiano kati ya China na Namibia na kutanufaisha ipasavyo watu wenyeji.

"China, kama ilivyo wakati wote, itaimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali na kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa pande mbili," amesema. 

Watu wakihudhuria ufunguzi rasmi wa Barabara ya John Mutorwa iliyojengwa na Kampuni ya China mjini Rundu, Namibia, Machi 14, 2025. (Picha na Musa Kaseke/Xinhua)

Watu wakihudhuria ufunguzi rasmi wa Barabara ya John Mutorwa iliyojengwa na Kampuni ya China mjini Rundu, Namibia, Machi 14, 2025. (Picha na Musa Kaseke/Xinhua)

John Mutorwa, naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Namibia, akizungumza kwenye ufunguzi rasmi wa Barabara ya John Mutorwa iliyojengwa na Kampuni ya China mjini Rundu, Namibia, Machi 14, 2025. (Picha na Musa Kaseke/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha