

Lugha Nyingine
Jeshi la Sudan latangaza kusonga mbele kwa sehemu kubwa katikati mwa Khartoum huku RSF ikikanusha
Jeshi la Serikali ya Sudan (SAF) limetangaza kuwa vikosi vyake vimesonga mbele kwa sehemu kubwa katikati ya mji mkuu Khartoum, kauli ambayo imekanushwa na Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF).
"Vikosi vyetu vimesonga mbele kwa sehemu kubwa katikati mwa Khartoum," msemaji wa SAF Nabil Abdalla amesema katika taarifa fupi.
Jeshi la Serikali pia limetoa taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, likitangaza kuwa vikosi vya jeshi hilo kutoka eneo la AL-Shajara, vikiungwa mkono na magari ya kijeshi, vimewafurusha kwa mafanikio wanamgambo wa RSF kutoka maeneo muhimu hadi kusini mwa sehemu ya kati ya Khartoum.
Hata hivyo, msemaji wa RSF El Basha Tabig amekanusha madai hayo, na kusema kuwa vikosi vya RSF vimeangamiza vikosi vya SAF vilivyojaribu kuvamia maeneo ya Sherwani, Nile Towers na Daraja la Al Mansheiya.
Habari zinasema Jeshi la Serikali linajaribu kuzingira vikosi vya RAF, vyenye kituo chake katikati mwa Khartoum na kuendelea kudhibiti maeneo muhimu, ikiwemo Ikulu na vituo vya kijeshi vilivyoko eneo la Al-Mogran.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma