

Lugha Nyingine
Ethiopia yatoa wito wa uungaji mkono wa kimataifa kuzuia mgogoro katika Jimbo la Tigray
Serikali ya Ethiopia imetoa wito wa uungaji mkono wa haraka wa jumuiya ya kimataifa kuepusha kutokea tena kwa mgogoro katika Jimbo la Tigray, kaskazini mwa nchi hiyo, ikilishutumu kundi moja la kisiasa kwa kukiuka mara kadhaa makubaliano ya amani yaliyomaliza vita vya miaka miwili.
Shirika la Habari la Ethiopia (ENA) limeripoti kuwa, waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Gedion Timothewos, ametoa taarifa kufuatia kuongezeka kwa mvutano ndani ya Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF), mtia saini wa Makubaliano ya Kudumu ya Kusitisha Uhasama (COHA), ambayo yalisaniniwa mwaka 2022 pamoja na serikali ya Ethiopia.
Akiongea Ijumaa iliyopita mjini Addis Ababa na jumuiya ya wanadiplomasia, waziri huyo amehimiza jumuiya ya kimataifa kutambua na kutofautisha wanaotaka kuharibu makubaliano ya COHA, na wale ambao wanajaribu kutekeleza kwa uaminifu makubaliano hayo na kuunga mkono mchakato kuendelea mbele.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma