

Lugha Nyingine
Kampuni za China zatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Zambia
Kampuni za China zinazofanya shughuli nchini Zambia zimetoa msaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo katika msimu wa mvua wa mwaka 2024/25.
Msaada huo wenye thamani ya dola za kimarekani elfu 42 unajumuisha chakula, viuatilifu, mablanketi, magodoro, vifaa vya kujikinga na vinginevyo. Mbali na vitu hivyo, kampuni hizo pia zimetoa mchango wa fedha taslimu za kwacha laki mbili (sawa na dola karibu elfu 7 za Marekani).
Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, Naibu Rais wa Zambia Bibi Mutale Nalumango amezishukuru kampuni hizo za China kwa msaada huo na kusema utapunguza kwa kiasi kikubwa machungu kwa waathirika.
Kwa mujibu wa naibu rais huyo, mafuriko hayo yamesababisha vifo vya watu wanne, na wengine wengi kupoteza makazi hasa mjini Lusaka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma