Idadi ya Wapalestina waliofariki yaongezeka hadi 413 huku mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2025

Wapalestina wakiomboleza watu waliofariki katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali katika Jiji la Gaza, Machi 18, 2025. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

Wapalestina wakiomboleza watu waliofariki katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali katika Jiji la Gaza, Machi 18, 2025. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

GAZA - Idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel katika maeneo mbalimbali kwenye Ukanda wa Gaza mapema jana Jumanne asubuhi imeongezeka hadi 413, mamlaka ya afya ya Gaza imesema. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baadaye siku hiyo, mamlaka hiyo ya afya imesema kuwa mashambulizi hayo ya Israel yanayoendelea pia yamejeruhi Wapalestina wasiopungua 562.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu kadhaa waliofariki au kujeruhiwa bado wamenasa chini ya vifusi na juhudi zinaendelea kuwaokoa.

Wakati huo huo, Jeshi la Israel na Shin Bet, shirika la upelelezi la Israel kwa pamoja wamesema mapema Jumanne mchana kwamba walikuwa wakiendelea kushambulia maeneo lengwa ya Hamas na Palestina Islamic Jihad kote Gaza.

"Kwa wakati huu, IDF (Vikosi vya Ulinzi vya Israel) na Shin Bet wanashambulia maeneo lengwa kote katika Ukanda wa Gaza," jeshi hilo na Shin Bet wamesema katika taarifa ya pamoja, wakiongeza kuwa "mashambulizi dhidi ya maeneo lengwa katika saa chache zilizopita yanajumuisha seli za magaidi, vituo vya kurusha roketi, maghala ya silaha, na miundombinu mingine ya kijeshi."

Israel imesema inarejesha mashambulizi kwa sababu ya ukataaji wa mara kwa mara wa Hamas kuwaachilia huru mateka wake na ukataaji wake mapendekezo yote iliyapokea kutoka kwa mjumbe wa rais wa Marekani Steve Witkoff na wapatanishi.

Hamas iliishutumu Israel kwa kukiuka masharti ya usimamishaji mapigano ulioanza Januari 19 na kutoa wito kwa wapatanishi kuishinikiza Israel kusitisha kampeni ya kijeshi. 

Mpalestina akiwa amebeba mwili wa mtu aliyefariki katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali katika Jiji la Gaza, Machi 18, 2025. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

Mpalestina akiwa amebeba mwili wa mtu aliyefariki katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali katika Jiji la Gaza, Machi 18, 2025. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

Wapalestina wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyefariki katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali katika Jiji la Gaza, Machi 18, 2025. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

Wapalestina wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyefariki katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali katika Jiji la Gaza, Machi 18, 2025. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha