Umoja wa Mataifa ahimiza pande hasimu za Sudan Kusini kukumbatia mazungumzo ili kuepusha kurejea katika vita

(CRI Online) Machi 19, 2025

Pande hasimu za Sudan Kusini zimetakiwa kuelekeza juhudi zote za kuzuia kurejea tena katika vita, kuunga mkono utekelezaji kamili wa makubaliano ya amani, na kuendeleza mpito kuelekea uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom, amesema jana Jumanne kuwa, Umoja huo una wasiwasi kuwa Sudan Kusini iko kwenye hatihati ya kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vinatishia kufuta mafanikio ya amani yaliyopatikana kwa bidii tangu kusainiwa kwa Mkataba uliohuishwa mwaka 2018.

Akiongea kwenye mkutano wa mtandaoni wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Sudan Kusini, Bw. Haysom amehimiza pande hasimu kupunguza mvutano wa sasa wa kisiasa bila kuchelewa, na kwa kwamba kuna njia moja tu ya kutoka katika mzunguko huo wa mgogoro, na njia hiyo ni Mkataba uliohuishwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha