

Lugha Nyingine
Ndege zilizoundwa China kuhimiza maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga Afrika
(CRI Online) Machi 19, 2025
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mashirika ya Ndege la Afrika Abderahmane Berthe amesema ujio wa ndege zilizoundwa na China kwenye soko la usafiri wa anga la Afrika unatarajiwa kuimarisha muunganiko, kupunguza gharama na kusaidia upanuzi wa mashirika ya ndege ya Afrika.
Bw. Berthe ameliambia shirika la habari la China, Xinhua kuwa sekta ya usafiri wa anga ya China inazalisha ndege zenye ufanisi mkubwa zinazotambulika kimataifa.
Akiongea pembezoni mwa Kongamano la Usafiri wa Ndege wa Kisasa la Afrika Bw. Berthe amesema upatikanaji wa ndege za kibiashara zilizoundwa China unatoa ufumbuzi wa kuimarisha ufanisi wa mashirika ya ndege ya Afrika.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma