

Lugha Nyingine
Kenya kuongeza kasi ya michezo ya magari ili kukuza utalii
(CRI Online) Machi 19, 2025
Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) imesema itatumia hamasa inayoongezeka kwenye mchezo wa mbio za magari kuongeza idadi ya wageni wanaokwenda kutalii Kenya.
KTB imesema mashindano ya WRC Safari Rally, yanayotarajiwa kuanza Alhamisi mjini Naivasha, yamekuwa mashindano muhimu katika kuifanya Kenya na ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na mvuto duniani.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa KTB Bi. June Chepkemei amesema mbio hizo za magari za WRC Safari Rally zimebadilika na kuwa jukwaa kuu la kuonyesha nguvu ya utalii ya Kenya kikanda na kimataifa.
Wapenzi takriban 30,000 wa mchezo wa mbio za magari kutoka Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, na Ethiopia watahudhuria mashindano hayo ya Naivasha, ikiwa ni ongezeko mara tatu kuliko 2024.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma