Timu ya wanasayansi inayoongozwa na China yafikia mawasiliano salama ya kwantamu ya 10,000 km ya kwanza duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2025

Picha hii, iliyotumwa kupitia mawasiliano salama ya kwantamu kati ya China na Afrika Kusini katika jaribio la usambazaji wa data, ikionyesha eneo la majaribio katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Afrika Kusini. (Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha China/ kupitia Xinhua)

Timu ya kimataifa inayoongozwa na wanasayansi wa China imefanikiwa kupata mawasiliano salama ya kwantamu ya kupita umbali wa kilomita zaidi ya 12,900 kati ya China na Afrika Kusini.

Mafanikio hayo mapya katika teknolojia ya kwantamu yameonyesha uwezekano wa mawasiliano salama ya kwantamu katika kiwango cha kimataifa.

Kwa mara ya kwanza duniani, timu hiyo inayoongozwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha China (USTC) imewezesha “usambazaji wa ufunguo wa kwantamu kwa wakati halisi” (real-time quantum key distribution, QKD) kati ya satalaiti na vituo vidogo vya ardhini, ikiwemo kimoja kilichopo Stellenbosch, Afrika Kusini.

Kwa kutumia mafanikio hayo, wanasayansi wa China, kwa kushirikiana na wenzao kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch, wameonyesha kwa mafanikio mawasiliano salama yenye kinga ya kudukuliwa ya kupita umbali mrefu zaidi hadi sasa.

Matokeo hayo yamechapishwa Jumatano wiki hii katika jarida la Nature. Mhakiki wa jarida hilo ameyasifu kama "mafanikio ya kuvutia kiufundi".

Picha hii ya Ukuta Mkuu inatumiwa katika majaribio ya utumaji wa data kupitia mawasiliano salama ya kwantamu kati ya China na Afrika Kusini. (Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha China/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha