Vizazi vitatu vya madaktari wa China na Gambia vyafanya upasuaji pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2025

Yang Qing (katikati, nyuma), mkurugenzi wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Shengjing ya Chuo Kikuu cha Tiba cha China, Cai Guiyang (mbele), mwanafunzi wa udaktari wa Yang na kiongozi wa kundi la 22 la timu ya madaktari wa China nchini Gambia, pamoja na Kebba Gassama (kushoto, nyuma), daktari wa uzazi katika Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis na Mariama Baye, muuguzi, wakifanya upasuaji usio wa maumivu makali, laparoscopic mjini Banjul, Gambia, Machi 17, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

Yang Qing (katikati, nyuma), mkurugenzi wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Shengjing ya Chuo Kikuu cha Tiba cha China, Cai Guiyang (mbele), mwanafunzi wa udaktari wa Yang na kiongozi wa kundi la 22 la timu ya madaktari wa China nchini Gambia, pamoja na Kebba Gassama (kushoto, nyuma), daktari wa uzazi katika Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis na Mariama Baye, muuguzi, wakifanya upasuaji wa laparoscopic usio wa maumivu makali mjini Banjul, Gambia, Machi 17, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

BANJUL - Alasiri ya Machi 17, katika chumba cha upasuaji cha magonjwa ya uzazi na wanawake cha Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis mjini Banjul, mji mkuu wa Gambia, mgonjwa mwenyeji wa ugumba alikuwa akisubiri upasuaji wake kwa hamu. Kulikuwa na uvimbe katika ovari yake ya kulia, hali iliyohitaji uchunguzi wa laparoscopic.

Daktari bingwa wa upasuaji aliyefanya upasuaji huo ni Yang Qing, mkurugenzi wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Shengjing ya Chuo Kikuu cha Tiba cha China.

Amefika Banjul siku mbili tu iliyopita Pamoja na wataalamu wengine wanne wa matibabu kwa programu ya wiki moja ya kutoa mafunzo. Programu hiyo, katika Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis, ni sehemu ya ushirikiano wa msaada wa matibabu kati ya nchi hizo mbili.

Msaidizi wa kwanza katika upasuaji huo ni Cai Guiyang, mwanafunzi wa daktari Yang. Cai sasa anaongoza kundi la 22 la timu ya madaktari wa China nchini Gambia.

Yang, mwenye umri wa miaka 61, amekumbushia kwamba Cai alianza utendaji wake wa kliniki mwaka 2010 na akaendelea hadi kutoa msaada wa matibabu katika maeneo ya vijijini mwaka 2019. "Kuona mwanafunzi wangu akikua na kuwa daktari wa kujitegemea, na hata kushiriki katika msaada wa kimataifa wa matibabu, hunijaza fahari na kuridhika sana," amesema.

Wengine waliosaidia katika upasuaji huo ni daktari bingwa wa uzazi katika hospitali hiyo Kebba Gassama na muuguzi Mariama Baye. Gassama na Baye waliopata mafunzo ya muda mfupi katika Hospitali ya Shengjing nchini China mwaka jana, wameendelea kupata uzoefu chini ya uelekezi wa Cai tangu waliporejea.

Sasa, vizazi vitatu hivyo vya washauri na wafunzwa vimesimama pamoja katika chumba cha upasuaji, vikifanya kazi ya kutibu wagonjwa wa Gambia.

Upasuaji huo pia umemfanya Yang kuona maendeleo yaliyofanywa na wataalamu wa matibabu wa Gambia. "Wakati wa vipindi vya mafunzo, walikuwa wakiangalia kutoka pembeni. Sasa, wanashiriki kikamilifu katika upasuaji. Labda katika siku za usoni, wataweza kufanya upasuaji kama huo kwa kujitegemea."

Upasuaji umekwenda vizuri, na kuondoa uvimbe wa ovari uliokuwa umeziba mrija wa uzazi, Cai amesema, shati lake likiwa limelowa jasho. "Kila operesheni ni fursa ya kujifunza. Hata kupotoka kidogo kutoka kwenye mpango wa upasuaji kunaonyeshwa mara moja."

Abdoulie Keita, mkuu wa idara ya uzazi na magonjwa ya wanawake katika Hospitali Ndogo ya Kufundisha ya Edward Francis, pia alishiriki kwenye mafunzo hayo ya muda mfupi katika Hospitali ya Shengjing, mwaka 2019. Kabla ya hapo, hakuwa na uzoefu wa upasuaji wa laparoscopic.

Muda mfupi baada ya kurejea Gambia, Keita ameweza kufanya upasuaji mdogo kwa kujitegemea.

"Hadi sasa, nimekamilisha upasuaji karibu 200 wa laparoscopic na hysteroscopic," amesema. "Ninawashukuru sana madaktari wa China kwa msaada wao."

Yang Qing (wa pili, kushoto), mkurugenzi wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Shengjing ya Chuo Kikuu cha Tiba cha China, Cai Guiyang (wa pili, mbele), mwanafunzi wa udaktari wa Yang na kiongozi wa kundi la 22 la timu ya madaktari wa China nchini Gambia, pamoja na Kebba Gassama (wa kwanza, kushoto), daktari wa uzazi katika Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis na Mariama Baye, muuguzi (wa kwanza kulia, mbele), wakifanya upasuaji wa laparoscopic mjini Banjul, Gambia, Machi 17, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

Yang Qing (wa pili, kushoto), mkurugenzi wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Shengjing ya Chuo Kikuu cha Tiba cha China, Cai Guiyang (wa pili kulia, mbele), mwanafunzi wa Yang na kiongozi wa kundi la 22 la timu ya madaktari wa China nchini Gambia, pamoja na Kebba Gassama (wa kwanza, kushoto), daktari wa uzazi katika Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis na Mariama Baye, muuguzi (wa kwanza kulia, mbele), wakifanya upasuaji wa laparoscopic mjini Banjul, Gambia, Machi 17, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

Yang Qing (wa pili, kushoto), mkurugenzi wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Shengjing ya Chuo Kikuu cha Tiba cha China, Cai Guiyang (wa kwanza, kulia), mwanafunzi wa udaktari wa Yang na kiongozi wa kundi la 22 la timu ya madaktari wa China nchini Gambia, pamoja na Kebba Gassama (wa kwanza, kushoto), daktari wa uzazi katika Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis na Mariama Baye, muuguzi (wa tatu, kushoto, mbele), wakifanya upasuaji walaparoscopic mjini Banjul, Gambia, Machi 17, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

Yang Qing (wa pili, kushoto), mkurugenzi wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Shengjing ya Chuo Kikuu cha Tiba cha China, Cai Guiyang (wa kwanza, kulia), mwanafunzi wa udaktari wa Yang na kiongozi wa kundi la 22 la timu ya madaktari wa China nchini Gambia, pamoja na Kebba Gassama (wa kwanza, kushoto), daktari wa uzazi katika Hospitali Ndogo ya Mafunzo ya Edward Francis na Mariama Baye, muuguzi (wa tatu, kushoto, mbele), wakifanya upasuaji walaparoscopic mjini Banjul, Gambia, Machi 17, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha