Serikali za Afrika zahimizwa kufanya biashara kwa kutumia sarafu za ndani

(CRI Online) Machi 21, 2025

Wataalamu waliohudhuria Mkutano wa 57 wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Kiuchumi wa Afrika wamehimiza serikali za Afrika kutafuta machaguo ya kukamilisha biashara na miamala mingine kwa fedha za ndani.

Mwanauchumi mkuu wa Kamisheni ya Kichumi Umoja wa Mataifa kwa Afrika, Hanan Morsy amesema kwenye mkutano huo kuwa, kutoa kipaumbele kwa fedha za ndani ni hatua ya haraka ya kulinda uchumi wa Afrika kutokana na misukosuko ya nje, na kuunda mfumo wa kifedha ulio na himilivu zaidi.

Mratibu wa Kituo cha Sera ya Biashara cha Afrika, Melaku Geboye Desta amesema, Afrika kufanya biashara kwa sarafu kama vile dola ya Marekani kunaligharimu bara hilo takriban dola bilioni 5 za Marekani kwa mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha