China yatoa msaada wa visima 66 kwa jamii za Zimbabwe zinazokabiliwa na changamoto ya maji

(CRI Online) Machi 21, 2025

China imekabidhi visima 66 kwa jamii katika Jimbo la Mashonaland Mashariki nchini Zimbabwe, na kuwezesha takriban watu 16,500 kupata maji safi.

Visima hivyo vilivyochimbwa na kampuni ya China, ni sehemu ya mradi wa kuchimba visima 300 kwa majimbo manne ya Zimbabwe.

Waziri wa Serikali za Mitaa na Ujenzi wa Umma wa Zimbabwe Bw. Daniel Garwe, amesema kwenye hafla ya makabidhiano kuwa visima hivyo si tu vitatoa maji salama kwa jamii zilizoathirika, bali pia vitatumika kama hatua ya kujenga uwezo wa kustahimili majanga katika siku za baadaye.

Pia amesema anaamini kuwa visima hivyo vitatumika kusaidia bustani za lishe na kuipatia mifugo maji hitajika.

Konsela wa masuala ya kiuchumi na kibiashara katika Ubalozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Huang Minghai, amesema mpango huo unaonyesha nguvu ya urafiki kati ya China na Zimbabwe, na dhamira ya pamoja ya kukabiliana na changamoto za uhaba wa maji na ukame.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha