

Lugha Nyingine
Mradi wa umwagiliaji unaojengwa na Kampuni ya China wabadilisha maisha ya wakulima wa Kenya
Ukiwa unajengwa na Kampuni ya China ya Sino Hydro, mradi wa Umwagiliaji wa Nzoia ya Chini ni mradi wa kitaifa ulio chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya Kenya. Umetekelezwa kuanzia Juni 2018, kwa lengo la kupunguza athari za mafuriko na kuongeza ukubwa wa ekari ya ardhi iliyo chini ya umwagiliaji magharibi mwa Kenya.
Ukiwa ni moja ya matawi yanayotiririsha maji katika Ziwa Victoria, ambalo ni ziwa kubwa zaidi la maji baridi barani Afrika, Mto Nzoia, ambao una urefu wa kilomita 257, ni chanzo cha shughuli za kujipatia mapato kwa mamilioni ya watu magharibi mwa Kenya.
Awamu ya kwanza ya mradi huo itakamilika Mei 2025, ikiweka ardhi ya ukubwa wa ekari 10,000 chini ya umwagiliaji kwenye kando ya kushoto ya mto huo na kunufaisha wakulima 12,600, Mamlaka ya Taifa ya Umwagiliaji, ambalo ni shirika la serikali la nchi hiyo imeeleza.
Awamu ya pili italeta ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 10,000 chini ya umwagiliaji katika upande wa kulia wa mto, huku wanufaika wakitarajiwa kuweka ardhi ya ukubwa wa ekari 5,000 chini ya mazao ya thamani ya juu na ardhi ya ukubwa wa ekari 5,000 chini ya mazao ya mpunga na mengineyo ya chakula, ikizalisha wastani wa shilingi bilioni 4.8 za Kenya (dola za Kimarekani milioni 37) katika mapato ya mwaka, shirika hilo limesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma