WHO yapongeza jitihada endelevu za Kenya katika kupambana na kifua kikuu

(CRI Online) Machi 25, 2025

Shirika la Afya Duniani (WHO) limepongeza jitihada endelevu za Kenya katika kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).

Mjumbe wa WHO nchini Kenya Diallo Abdourahmane ameisema jana Jumatatu kuwa Kenya imepata maendeleo makubwa ambapo katika nchi saba duniani zinazobeba mzigo mkubwa wa Kifua Kikuu, Kenya imepunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 41, na vifo kwa asilimia 60 katika mwaka 2023.

Amesema Kenya inaendelea kutafuta njia katika kumaliza tatizo hilo kwa kuongeza vifaa vya kidigitali, ugunduzi haraka wa ugonjwa, na mpango wa matibabu wenye ufanisi zaidi, huku ikikumbatia uvumbuzi.

Ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaathiri usalama wa chakula, na kusababisha utapiamlo pamoja na kuzidisha uwezekano wa maambukizi ya Kifua Kikuu, nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kujitahidi zaidi kwenye usimamizi wa Kifua Kikuu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha