

Lugha Nyingine
Tanzania yapunguza maambukizi mapya ya Kifua Kikuu kwa asilimia 40 katika kipindi cha miaka minane
Tanzania imeungana na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani (TB), ikisema kuwa serikali ya nchi hiyo imefanikiwa kupunguza maambukizi mapya ya Kifua Kikuu kwa takriban asilimia 40 katika kipindi cha miaka minane.
Kwenye taarifa ya kuadhimisha siku hiyo inayoangukia Machi 24 kila mwaka aliyoitoa katika Ikulu ya Dodoma, mji mkuu wa nchi hiyo ili kuongeza udharura wa kutokomeza ugonjwa huo wa kifua kikuu, Naibu Waziri wa Afya wa Tanzania, Dokta Godwin Mollel amesema maambukizi mapya ya Kifua Kikuu yalipungua kutoka wagonjwa 306 kwa kila watu 100,000 mwaka 2015 hadi wagonjwa 183 kwa kila watu 100,000 mwaka 2023.
Mollel amebainisha kuwa vifo vinavyotokana na TB vimepungua kutoka 56,000 mwaka 2015 hadi 18,400 mwaka 2023, ikiwa ni sawa na punguzo la asilimia 67.
Mollel amesema jambo hilo limeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 13 duniani zenye lengo la kupunguza vifo vinavyotokana na Kifua Kikuu kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2025, kulingana na makadirio ya Shirika la Afya Duniani (WHO).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma