

Lugha Nyingine
Wataalamu wakutana Kenya ili kuhimiza usimamizi wa taka za kielektroniki katika Afrika Mashariki
Wataalamu kutoka kote Afrika Mashariki wamekusanyika mjini Nairobi, Kenya siku ya Jumatatu kujadili njia za kuhimiza usimamizi endelevu wa taka za kielektroniki katika kanda hiyo.
Mkutano huo wa saba wa Uhamasishaji wa Kikanda wa Shirika la Mawasiliano la Afrika Mashariki (EACO) kuhusu Usimamizi Endelevu wa taka za kielektroniki katika Kanda ya Afrika Mashariki umewaleta pamoja washiriki zaidi ya 100, wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wadhibiti wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na wadau wa sekta hiyo, ili kupunguza taka za kielektoroniki katika kanda hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali ya Kenya, John Tanui, amesema uuzaji wa vifaa vya umeme na kielektroniki, kama vile mafriji, televisheni, na simu za mkononi, utaendelea kuongezeka, na kutokana na kudumu kwa muda mfupi, ongezeko kubwa la taka za kielektroniki linatarajiwa barani Afrika.
Naye Katibu Mtendaji wa EACO Ally Simba, ameibainisha kuwa taka za kielektroniki bado zinaongezeka kwa kasi zaidi barani Afrika. Hata hivyo, kanda haina hiyo miundombinu ya kutosha ya kuchakata na kuzalisha bidhaa za mzunguko ili kukabiliana na changamoto hiyo ipasavyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma