

Lugha Nyingine
Viongozi wa Afrika wateua wapatanishi watano wa amani kwa ajili ya mchakato wa amani nchini DRC
Viongozi wa Afrika kutoka mashariki na kusini mwa Afrika wa,wameteua marais watano wastaafu kwenye jopo lililopanuliwa la wapatanishi ili kuendeleza mchakato wa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mkutano wa kilele uliofanyika juzi Jumatatu jioni.
Marais hao wastaafu walioteuliwa kwenye jopo hilo ni pamoja na wa Nigeria Olusegun Obasanjo, wa Kenya Uhuru Kenyatta, wa Afrika Kusini Kgalema Motlanthe, wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba Panza na wa Ethiopia Sahle-Work Zewde.
Mkutano huo ulioongozwa na Rais wa Kenya William Ruto na mwenzake wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa uliwaleta pamoja viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Katika hotuba yake, Ruto alisema viongozi kutoka jumuiya hizo mbili za kikanda wamedhamiria kushughulikia mgogoro unaoongezeka ambao umesababisha watu kupoteza maisha, maelfu kukimbia makazi yao na janga baya la kibinadamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma