

Lugha Nyingine
Jeshi la Uganda lasema utulivu umerejea DRC baada ya mapigano makali
(CRI Online) Machi 26, 2025
Jeshi la Uganda limesema wanajeshi wake waliotumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), haswa katika mji wa Bunia, wamesaidia kuzuia mauaji ya raia.
Kaimu msemaji wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi la Uganda (UPDF) Chris Magezi amesema kuwa uwepo wa vikosi vya Uganda huko Bunia, Djugu, na Mahagi umeimarisha kwa kiasi kikubwa usalama katika Jimbo la Ituri, kaskazini mwa DRC.
Uganda ilituma wanajeshi wiki kadhaa zilizopita ili kuzuia mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha wa Lendu walioko chini ya Kundi la Ushirika wa Maendeleo ya Kongo (CODECO) na wanamgambo wengine.
Ujumbe huo pia unalenga kuzuia waasi wa Vikosi vya Muungano wa Kidemokrasia (ADF) kuingia katika eneo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma