Shirika la Ndege la Kenya lapata faida kwa mara ya kwanza katika miaka 11 iliyopita

(CRI Online) Machi 26, 2025

Shirika la Ndege la Kenya (KQ) limesema baada ya kupata hasara kwa zaidi ya muongo mmoja, sasa limepata faida ya dola takriban milioni 41.7 za kimarekani, katika mwaka wa fedha ulioishia mwezi Desemba 2024, ikijitoa kutoka kwenye hasara ya dola milioni 174.6 za kimarekani ya mwaka 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Allan Kilavuka amesema Jumanne kuwa, faida hiyo inaonyesha mabadiliko makubwa, ikiwa imeongezeka kwa dola 216.3 za kimarekani.

Amebainisha kuwa shirika lake linaendelea kuvutia wawekezaji wa kimkakati, ili kuhakikisha hali endelevu ya muda mrefu.

Amesema, ingawa sekta ya usafiri wa anga inakabiliwa na changamoto duniani, kama vile uhaba wa ndege, injini na vipuri, lakini mkakati wake wa mageuzi unapata matokeo mazuri.

Mwenyekiti wa KQ Michael Joseph amesema matokeo hayo si tu yanaweka rekodi ya idadi kubwa zaidi ya abiria na mapato makubwa katika historia ya shirika hilo, bali pia yanathibitisha uwezo wake mkubwa wa uendeshaji na ustahamilivu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha