

Lugha Nyingine
Afrika Mashariki yazindua programu ya mafunzo ya usimamizi wa data kwa majaji
Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) wamezindua mpango wa kiuvumbuzi wa mafunzo ya usimamizi wa data kwa maafisa wa mahakama.
Kwa mujibu wa taarifa ya EAC iliyotolewa Jumatano, uzinduzi wa programu hiyo, pamoja na mafunzo yake ya kwanza yaliyofanyika Machi 11 hadi Machi 13 mjini Kigali, nchini Rwanda, ni hatua muhimu katika kuimarisha utaalamu wa mahakama juu ya usimamizi wa data, faragha, na uamuzi wa kisheria.
Taarifa imeongeza kuwa kuinuka kwa uchumi wa kidijitali kumefanya usimamizi wa data kuwa suala muhimu kwa kanda hiyo ya Afrika Mashariki.
Imeeleza kuwa, programu hiyo imeandaliwa ili kuwapa majaji ujuzi na maarifa hitajika katika kutafsiri na kutekeleza Sheria ya Faragha na Ulinzi wa Data ya EAC inayopendekezwa na kuhakikisha mbinu ainishi ya kikanda ya usimamizi wa data katika zama ya teknolojia inayoibuka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma