

Lugha Nyingine
UN: Majeruhi wa shambulizi dhidi ya soko la Sudan wanakufa kutokana na ukosefu wa matibabu
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema waathirika kadhaa wa mashambulizi ya anga dhidi ya soko la Tora, yaliyosababisha mamia ya vifo na majeruhi katika Jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, wanakufa kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu huko El Fasher, ambako taasisi nyingi za afya zimelazimika kufungwa kutokana na uhasama na kuzingirwa kunakoendelea.
Mratibu mkaazi wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Clementine Nkweta-Salami amelaani mashambulizi yote ya kimakusudi na ya kiholela dhidi ya raia.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Turk amesema kuwa ameshangazwa na ripoti kwamba mamia ya raia wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Jeshi la Sudan dhidi ya soko lenye umati mkubwa wa watu.
Amehimiza tena ulinzi wa raia na njia salama kwa wale wanaokimbia maeneo yenye migogoro. Pia amesisitiza kuwa, ufikiaji wa misaada ya kibinadamu lazima uhakikishwe ili watu wote walioko Darfur Kaskazini wapate kile wanachohitaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma