WFP: Wakimbizi zaidi ya 170 wa DRC wamekimbilia Tanzania tangu mwanzoni mwa mwaka 2025

(CRI Online) Machi 27, 2025

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuwa wakimbizi 171 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekimbilia Tanzania tangu mwanzoni mwa mwaka 2025 kutokana na msukosuko wa kibinadamu jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC.

WFP imesema katika taarifa yake ya Jumanne kuwa idadi ya wakimbizi kutoka DRC inatarajiwa kuongezeka kutokana na mapambano yanayoendelea kati ya jeshi la DRC na kundi la waasi la M23.

Ingawa idadi hiyo ni ndogo, lakini WFP na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) yameweka mpango wa kukabiliana na hali ya dharura unaoendana na mwelekeo wa nchini Burundi, Rwanda na Uganda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha