Viongozi wa Turkana nchini Kenya wapinga mpango jumuishi wa wakimbizi katika jamii

(CRI Online) Machi 31, 2025

Wazee kutoka jamii ya Turkana, kaskazini mwa Kenya, wamepinga mpango uliozinduliwa na rais wa nchi hiyo William Ruto Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita, ambao unalenga kuwajumuisha wakimbizi kutoka nchi jirani katika jamii za huko.

Mbunge wa Jimbo la Turkana Magharibi, Daniel Epuyo, amewaongoza wazee wa huko katika kupinga mpango huo unaoitwa Mpango wa Shirika, akisema jamii za huko hazijashauriwa kuhusu mpango huo, na pia hakuna huduma muhimu za kijamii.

Viongozi wa kaunti ya Turkana wameonya kuwa, mpango huo unaweza kusababisha vurugu na jamii zinazowapokea ambazo tayari zinakabiliwa na uhaba wa maji na chakula.

Kaunti ya Turkana ni makazi ya kambi za wakimbizi za Kakuma na Kalobeyei, ambazo ziko mpakani na Sudan Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha