Namna teknolojia ya kilimo ya China inavyokuwa "msimbo kwa mavuno mazuri" barani Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2025

Wakulima wenyeji wakivuna mpunga kwenye shamba kielelezo la mpunga chotara wa mazao mengi, Mahitsy, Madagascar, Mei 8, 2024. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Wakulima wenyeji wakivuna mpunga kwenye shamba kielelezo la mpunga chotara wa mazao mengi, Mahitsy, Madagascar, Mei 8, 2024. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

NAIROBI/BEIJING - Noti ya ariary ya 20,000 ya Madagascar ina mchele chotara, ishara ya ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika.

Tangu mwaka 2007, China imekuwa ikituma wataalam wa kilimo nchini Madagascar, ikiongeza kwa mafanikio mavuno ya mpunga kwenye mashamba ya kielelezo hadi mara mbili au tatu ya aina za jadi za mpunga wa Afrika.

Hadi kufikia mwaka 2022, teknolojia hiyo ilikuwa imetumiwa kwenye mashamba yenye ukubwa wa hekta 75,000, ikiongeza maradufu mapato ya makumi ya maelfu ya wakulima na kwa kiasi kikubwa kuimarisha uwezo wa Madagascar wa kujitosheleza kwa chakula.

Katika nchi nyingi za Afrika, usalama wa chakula na maendeleo ya kilimo bado vinaendelea kuwa masuala yanayohitaji msukumo mkubwa. Katika miaka ya hivi karibuni, bara hilo limebadilika kutoka "kutegemea hali ya hewa kwa mazao mazuri" hadi "kupata mavuno mazuri kwa kutumia teknolojia," kutokana na ujuzi wa kilimo kutoka China.

Kubadilika teknolojia kulingana na hali ya huko

Msingi wa utekelezaji wa teknolojia upo katika "kubadilika kuendana na hali ya eneo husika." Wataalamu wa China wanazifanya kimahsusi programu zao ili kuendana na sifa za kipekee za udongo na tabianchi barani Afrika.

Nchini Guinea-Bissau, kwa mfano, mbinu inayojumuisha "teknolojia na vifaa" imepokelewa vyema na wenyeji. China imetoa msaada wa vitu katika mfumo wa mashine na zana za kilimo huku ikituma wataalamu wa kilimo kutoa mafunzo ya muda mrefu ya kiufundi.

“Hii imeongeza ipasavyo idadi ya wafanyakazi wenye ujuzi wa kilimo,” anasema Mamadu Saliu Lamba, waziri wa zamani wa kilimo, misitu na maendeleo vijijini wa nchi hiyo.

Kati ya mwaka 2013 na mwisho wa mwaka 2023, China ilianzisha vituo 24 vya kielelezo vya teknolojia ya kilimo barani Afrika na kuleta teknolojia za hali ya juu za kilimo zaidi ya 300, ikiongeza mavuno ya mazao ya kienyeji kwa wastani wa asilimia 30 hadi 60 na kunufaisha wakulima zaidi ya milioni 1 katika bara zima.

Kulingana na hali ya sehemu husika, kilimo cha mpunga chotara, pamoja na teknolojia nyingine za kilimo cha China, vimekuwa njia muhimu ya kusaidia nchi za Afrika kupambana na umaskini na kupata kujitosheleza kwa chakula.

Zhang Hong'en, mkurugenzi wa Kituo cha Kielelezo cha Mifugo nchini Mauritania, akikagua ukuaji wa nyasi ya Juncao kwenye shamba la majaribio katika kijiji cha Idini nchini Mauritania, Januari 18, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

Zhang Hong'en, mkurugenzi wa Kituo cha Kielelezo cha Mifugo nchini Mauritania, akikagua ukuaji wa nyasi ya Juncao kwenye shamba la majaribio katika kijiji cha Idini nchini Mauritania, Januari 18, 2025. (Xinhua/Si Yuan)

Kuhimiza maendeleo kupitia uvumbuzi

Kilomita takriban 60 mashariki mwa mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott, kijiji cha Idini, kwenye ukingo wa Jangwa la Sahara, awali kilikuwa kikikumbwa na joto kali, ukame, udongo duni na dhoruba kali za mchanga.

Leo, teknolojia ya China ya kukuza uyoga inayojulikana kwa jina la "Juncao" -- maneno ya kichina yanayomaanisha "uyoga" na "nyasi" -- imekita mizizi hapa.

"Kondoo wetu walikuwa wakifa njaa au kudhoofika," amekumbushia Amir Abdou, mfugaji mwenyeji, ambaye wakati fulani alipata kuhangaika na jangwa.

"Shukrani kwa wataalamu wa China waliotufundisha kukuza Juncao na mimea mingine, hatimaye tuna malisho ya kulisha mifugo yetu. Leo, ninafuga kondoo 10, wote wakiwa na afya bora. Asante, marafiki wa China!" Amesema.

Uvumbuzi kama huo wa kiteknolojia kama vile wa mashine ndogo za kilimo ambazo hupunguza uharibifu wa udongo kupitia kilimo cha usahihi na aina za mpunga zinazostahimili ukame na mafuriko umeleta suluhu endelevu kwa changamoto za kilimo barani Afrika.

Ushirikiano wa kunufaishana

Mwezi Agosti 2022, parachichi freshi za Afrika zilisafirishwa nchini China kwa mara ya kwanza, ikionyesha ushirikiano wa kina na wa hali mbalimbali wa kilimo kati ya pande hizo mbili.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa mwaka 2024, China imeanzisha utaratibu wa ushirikiano wa kilimo na nchi 23 za Afrika na mashirika ya kikanda, na kutia saini mikataba 72 ya ushirikiano.

Kampuni za kilimo cha biashara zaidi ya 200 za China sasa zinafanya kazi barani Afrika, huku uwekezaji wa jumla wa China kwenye kilimo katika bara hilo ukizidi dola za Kimarekani bilioni 1. Hii imeunda mtandao shirikishi unaohusisha kilimo, usindikaji na biashara.

Mtaalamu wa China Luo Zhongping (katikati) akizungumza na wakulima wa mpunga wakati wa kutembelea shamba la mpunga, Butaleja, mashariki mwa Uganda, Agosti 15, 2023. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Mtaalamu wa China Luo Zhongping (katikati) akizungumza na wakulima wa mpunga wakati wa kutembelea shamba la mpunga, Butaleja, mashariki mwa Uganda, Agosti 15, 2023. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Mbali na wataalam wa China wanaotumwa Afrika, wanafunzi wa Afrika waliosoma nchini China pia wametoa mchango kutumia teknolojia hizo katika bara zima.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha