

Lugha Nyingine
Ethiopia yazindua chanjo dhidi ya kipindupindu kwa watu milioni 1 walio hatarini
Serikali ya Ethiopia imezindua kampeni ya chanjo dhidi ya kipindupindu katika sehemu ya kusini magharibi mwa nchi hiyo, ikilenga watu milioni moja walio hatarini.
Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Wizara ya Afya ya nchini humo imesema chanjo hiyo itatolewa katika kanda zote za Jimbo la Gambella na kambi za wakimbizi katika wiki hii.
Hatua hiyo inakuja wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) na mashirika mengine ya kibinadamu yakitoa wito wa juhudi za pamoja ili kudhibiti mlipuko wa kipindupindu unaoenea kwa kasi katika jimbo hilo la Gambella lililo jirani na Sudan Kusini.
Waziri wa Afya wa Ethiopia Mekdes Daba amesema, licha ya kupanua upatikanaji wa chanjo dhidi ya kipindupindu, kudumisha usafi binafsi na wa mazingira ni hatua muhimu katika kuzuia milipuko ya ugonjwa huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma