

Lugha Nyingine
China na Zambia zasaini makubaliano ya kuuza karanga pori
China na Zambia zimesaini makubaliano ya kuuza karanga pori nchini China ambapo hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika jana Jumatatu, ilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo wa Zambia Mtolo Phiri na Balozi Mdogo wa Ubalozi wa China nchini Zambia Wang Shen.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri Phiri ameishukuru China kwa kuipatia Zambia soko la wazi na kubwa kwa ajili ya zao lake la karanga pori.
Amesema hatua hiyo itasaidia Zambia kuwa na kuanuwaisha uzalishaji wa kilimo na kuboresha ubora wa bidhaa zake, kwa kuwa China inadumisha vigezo vya juu kwa bidhaa za kilimo zinazoingizwa nchini humo.
Naye Balozi Wang amesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo ni hatua muhimu katika kufungua soko la China kwa karanga zinazotoka Zambia, ambayo itanufaisha sana wakulima wa Zambia katika siku zijazo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma