

Lugha Nyingine
China yasema mazoezi ya kijeshi karibu na Kisiwa cha Taiwan ni vitendo halali vya kulinda mamlaka ya nchi ya China
BEIJING – Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China jana Tarehe Mosi alisema, mazoezi ya kijeshi yanayofanyika kwenye eneo karibu na Kisiwa cha Taiwan ni onyo kali na kitendo cha kuzuia nguvu ya mafarakano ya kutaka "Taiwan Ijitenge", na operesheni halali na muhimu ya kulinda mamlaka ya nchi na kudumisha Muungano wa Taifa.
Eneo la kivita la mashariki la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) jana Jumanne lilianza kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwenye eneo lililo karibu na kisiwa cha Taiwan.
Akijibu swali husika, Guo amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba Taiwan ni sehemu isiyotengeneka ya ardhi ya China, na suala la Taiwan ni mambo ya ndani kabisa ya China yasiyoruhusu uingiliaji kutoka nje.
Utawala wa Chama cha Kidemokrasia cha Maendeleo umefanya chini juu kutafuta "Taiwan Ijitenge," na kujaribu kuomba uungaji mkono kutoka nje kwa ajenda hiyo na kujaribu kufarakanisha nchi, amesema msemaji huyo.
Guo amesema, "Jaribio kama hilo ni bure na linaishia kufeli vibaya," na " China itafanikiwa na lazima ifikie muungano, huu ni mwelekeo usiozuilika”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma