Eneo la Pembe ya Afrika lapokea wakimbizi milioni 24.5

(CRI Online) April 02, 2025

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) wamesema katika ripoti kuwa, idadi ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi wa ndani katika eneo la Pembe ya Afrika imefikia milioni 24.5 hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi.

Mashirika hayo yamesema, idadi hiyo ilipungua kutoka milioni 26.3 kutokana na kurejeshwa kwa wakimbizi nchini kwao na kuboreshwa kwa usalama katika baadhi ya nchi zilizoathiriwa, wakisema hali ya usalama imeboreshwa nchini Sudan na kuruhusu wakimbizi kurudi kutoka nje ya nchi na Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kati ya watu hao milioni 24.5, milioni 18.9 ni wakimbizi wa ndani, na watu milioni 5.6 ni wakimbizi kutoka nje ya nchi na wanaotafuta hifadhi.

Sababu kuu kwa watu kukimbia makazi yao katika kanda hiyo ni pamoja na migogoro, athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile mafuriko na ukame, na ukosefu wa usalama wa chakula.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha