

Lugha Nyingine
China yaitaka Ufilipino kutochochea moto juu ya suala la Taiwan
BEIJING - China inawataka watu fulani nchini Ufilipino wasichochee moto juu ya suala la Taiwan, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Guo Jiakun amesema.
Msemaji Guo amesema hayo jana Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari akijibu swali la vyombo vya habari kuhusu maneno aliyosema hivi karibuni mkuu wa jeshi la Ufilipino kwamba bila shaka Ufilipino haitaweza kuepusha kuhusika kama kutakuwa na mgogoro juu ya Taiwan, na pia amedai kwamba China inajipenyeza kwa juhudi katika taasisi za Ufilipino, likiwemo jeshi.
Guo amesema, "Suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China na liko kiini katika kiini cha maslahi ya China," na "Kutatua suala la Taiwan ni jambo la Wachina wenyewe ambalo hakuna mtu anayeruhusiwa kuliingilia."
Msemaji huyo amesema, "Tunawata watu fulani nchini Ufilipino wasichochee moto juu ya suala la Taiwan, na wanaochochea moto hakika wataangamizwa nao," na China pia inapinga watu husika kujaribu kufanya udanganyifu na kutoa shutuma zisizo na msingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma