

Lugha Nyingine
Zaidi ya watu 970 wasaini azimio la kuping sera ya ushuru ya Marekani
Zaidi ya watu 970 wakiwemo wachumi waandamizi duniani wamesaini azimio la kupinga ushuru, wakikosoa sera ya ushuru iliyoanzishwa na serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump kuwa haina mwongozo, huku wakionya uwezekano wa kudimimia kwa uchumi wa nchi hiyo.
Ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari zimesema, barua hiyo iliyosainiwa na wachumi maarufu akiwemo mshindi wa tuzo ya Nobel James Heckman na Vernon Smith, ilikuwa ikizunguka mtandaoni mwishoni mwa wiki, na mpaka kufikia jana Jumapili alfajiri, ilikuwa imeshasainiwa na watu 970.
Katika barua hiyo, waandishi wamepinga sera ya ushuru wa reciprocal (kutozana sawa) iliyopendekezwa na Rais Trump ambayo inaathiri nchi na maeneo zaidi ya 180 duniani.
Barua hiyo imesema, kiwango cha ushuru huo kinahesabiwa kwa kutumia mfumo mbaya na usio sahihi, na msingi katika uhalisia wa kiuchumi.
Tarehe 2 mwezi huu, Rais Trump alitangaza mfululizo wa ushuru dhidi ya washirika wa kibiashara wa Marekani, akiita siku hiyo kuwa ni 'Siku ya Ukombozi.'
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma