

Lugha Nyingine
China yapinga vikali ujanja wa kisiasa wa Marekani juu ya utafutaji chanzo cha UVIKO-19
BEIJING - Kurejelea hoja ya "uvujaji wa kutoka maabara" kwenye tovuti husika na kuichafua China kwa shutuma zisizo na uthibitisho ni mbinu nyingine tu ambayo Marekani inafanya ujanja wa kisiasa kwa kisingizio cha kutafuta chanzo cha UVIKO-19, Guo Jiakun msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema jana Jumanne, akisema kuwa China inapinga vikali kitendo hiki.
Wikiendi iliyopita, Ikulu ya White House ilianzisha tovuti mpya ambayo inakusudia kueleza chanzo cha janga la UVIKO na kusema kwamba "janga hilo lilianzia kwenye uvujaji wa kutoka maabara nchini China."
Akijibu swali husika, msemaji Guo ameuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba ufuatiliaji wa chanzo cha virusi ni suala kubwa la kisayansi na China ikiwa na moyo wa kufuata njia ya kisayansi, wazi na bila kuficha, imekuwa ikiunga mkono na kufanya juhudi za kushiriki katika ufuatiliaji chanzo kwa njia ya kisayansi.
Ameitaka Marekani kuacha mara moja kuingiza siasa katika utafutaji wa chanzo cha virusi na kuutumia kuwa silaha, kuacha kuwafanya wengine kuwa mbuzi wa kafara, na kuacha kujifanya kiziwi kwa maswali kuhusu kazi yake katika janga hilo.
"Marekani bado inawiwa na jumuiya ya kimataifa jibu makini kwa wasiwasi huo halali, na maelezo ya kuwajibika kwa watu wa dunia," Guo amebainisha.
"Tangu janga hilo lianze, tumeona ripoti nyingi za vyombo vya habari kuhusu tetesi zinazokuwa zimepatikana katika maeneo na nchi nyingi kote duniani juu ya uwezekano wa chanzo cha virusi," msemaji huyo amesema, akisema kuwa Marekani ni moja ya maeneo hayo, na wakati fulani iliwahi kukumbwa na Ugonjwa wa Uharibifu wa Mapafu na suala la Maabara ya Biolojia ya Fort Detrick.
"Tunaamini kwamba jumuiya ya kimataifa inastahili maelezo wazi kutoka upande wa Marekani," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma