Waziri wa Mambo ya Nje wa China atoa wito kwa China na Uingereza kushikilia utaratibu wa kimataifa ulioanzishwa baada ya WWII

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2025

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo kwa njia ya simu jana Jumanne na mwenzake wa Uingereza David Lammy, akisema kuwa, katika hali ya hivi sasa ya kukithiri kwa vitendo vya umwamba vya upande mmoja, China na Uingereza zina wajibu wa kulinda utaratibu wa kimataifa ulioanzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema pande hizo mbili pia zina wajibu wa pamoja wa kulinda mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa na kulinda mfumo wa biashara za pande nyingi.

Wang amedhihirisha kuwa mwelekeo wa kupunguza hali wasiwasi ya uhusiano kati ya China na Uingereza haujapatikana kirahisi na unahitaji kuthaminiwa zaidi, China inapenda kushirikiana na Uingereza katika kuondoa mivurugano na mikengeuko mbalimbali na kuongoza uhusiano wa pande mbili kufuata mwelekeo wa kuendelea kwa hatua madhubuti.

Wang amesema kuwa Marekani kutumia ushuru kama silaha ya kufanya mashambulizi dhidi ya nchi mbalimbali bila tofauti, kitendo chake hiki hakiwezi kupata uungaji mkono wa watu na kitashindwa kuendelea.

China ikiwa nchi kubwa inajitokeza kuipinga Marekani kutumia ushuru kama silaha, si kama tu China inalenga kulinda haki na maslahi yake halali, bali pia inalenga kulinda kanuni za kimataifa na mfumo wa biashara wa pande nyingi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha