China yatoa msaada wa tani 2,400 za mchele kwa Togo

(CRI Online) April 23, 2025

China imekabidhi shehena ya mwisho ya msaada wa mchele kwa serikali ya Togo jana Jumanne katika hafla iliyofanyika kwenye Kurugenzi ya Kikanda ya Masuala ya Baharini iliyo chini ya Mamlaka ya Taifa ya Usalama wa Chakula ya nchi hiyo.

Katika hafla ya makabidhiano ya shehena hiyo katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Togo Afo Salifou amesema, msaada huo unaonyesha nguvu ya ushirikiano kati ya China na Togo, na kueleza matumaini yake kwamba, ushirikiano huo utaendelea kuwa wa kina zaidi katika maeneo mengine ikiwemo afya, uwekezaji na ujenzi wa miundombinu.

Naye Balozi wa China nchini Togo Chao Weidong amesema, mradi huo wa dharura wa chakula ni moja ya mafanikio ya ushirikiano wa pande mbili kufuatia Mkutano wa Kilele wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing mwaka jana.

Msaada huo unajumuisha tani 2,400 za mchele mweupe wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2.74, na ni sehemu ya mradi wa msaada wa chakula unaolenga kuimarisha uhimilivu wa chakula kwa wananchi wa Togo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha