Thamani ya Biashara ya China ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa kwa Kenya yaweka rekodi mpya katika historia

(CRI Online) April 23, 2025

Takwimu kutoka Idara Kuu ya Forodha ya China zimeonesha kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara ya China ya uagizaji na uuzaji bidhaa nje kwa Kenya ilifikia dola za kimarekani bilioni 2.2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, ongezeko hilo limedumishwa kwa robo sita mfululizo. Miongoni mwa bidhaa hizo, uuzaji wa bidhaa nje uliongezeka kwa asilimia 11.8, na uagizaji wa bidhaa uliongezeka kwa asilimia 13.2.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha