Kenya yaanzisha mradi wa kujenga uwezo dhidi ya ufadhili kwa makundi ya kigaidi

(CRI Online) April 23, 2025

Wizara ya Ulinzi ya Kenya imezindua mradi wa mafunzo kwa maofisa wa mashirika ya usimamizi utekelezaji wa sheria jana Jumanne mjini Nairobi katika kubaini, kuripoti na kuzuia ufadhili na utakatishaji fedha kwa makundi ya kigaidi.

Ukiwa umeungwa mkono na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Kiislamu katika Kupambana na Ugaidi (IMCTC), muungano wa kijeshi wa nchi 42 wa kupambana dhidi ya ugaidi wenye makao yake mjini Riyadh, Saudi Arabia, mpango huo wa ujengaji uwezo una lengo la kuvuruga ufadhili kwa taasisi zinazochochea itikadi kali na utakatishaji wa fedha.

Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Soipan Tuya, amesema ugaidi umeendelea kuwa tishio la amani, usalama na maendeleo ya kikanda, akiongeza kuwa, ufadhili kwa makundi ya kigaidi unachochea uandikishaji, mipango, ugavi na operesheni za kigaidi.

Amesema bila ya kukabiliana na ufadhili wa kifedha unaodumisha mitandao hiyo, juhudi pana za kupambmana dhidi ya ugaidi zitakuwa hatarini kufanikiwa.

Katibu Mkuu wa IMCTC Mohamed bin Saeed Al-Moghedi amesema, Kenya iko katika sehemu ya kimkakati kuunga mkono juhudi za kikanda katika kupambana dhidi ya ugaidi kwa kutumia vifaa vya kisera, kisheria, na fedha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha