Mlipuko wa nzige wathibitishwa kaskazini mashariki mwa Namibia

(CRI Online) April 23, 2025

Wizara ya Kilimo, Uvuvi, Maji na Mageuzi ya Ardhi nchini Namibia imethibitisha kutokea kwa mlipuko wa nzige katika mkoa wa Zambezi ulioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ukiathiri maeneo mengi na kuleta wasiwasi wa uwezekano wa wimbi la pili la uvamizi wa nzige hao.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne, mkurugenzi mkuu wa Wizara hiyo Ndiyakupi Nghituwamata amesema, mlipuko huo kwa mara ya kwanza uliripotiwa mwanzoni mwa mwezi Februari kufuatia mvua kubwa zilizonyesha.

Amesema nzige wameonekana katika kanda za mafuriko za Ibbu, karibu na Mto Chobe, na pia katika kanda 11 za mkoa wa Zambezi, na kuongeza kuwa, mvua kubwa zimetoa mazingira mazuri kwa nzige hao kuzaliana.

Amehimiza wakulima kutoa ripoti mara moja kwa Kituo cha Maendeleo ya Kilimo kilicho karibu mara wanapoona kundi la nzige ama wadudu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha