Spika wa Bunge la China akutana na Rais wa Kenya

(CRI Online) April 24, 2025

Spika wa Bunge la Umma la China Bw. Zhao Leji amekutana na Rais wa Kenya William Ruto jana Jumatano mjini Beijing ambaye yupo ziarani nchini China.

Bw. Zhao amesema, bunge la umma la China liko tayari kushirikiana na bunge la Kenya kutumia vyema utaratibu wa mawasiliano kati ya taasisi hizo za utungaji sheria katika kuimarisha mabadilishano kati ya ngazi mbalimbali, na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali zikiwemo sheria, usimamizi na ulinzi wa mazingira ya ikolojia, ili kutoa hakikisho la kisheria kwa ajili ya ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Rais Ruto amesisitiza kuwa, Kenya inapenda kuimarisha ushirikiano na China katika sekta za uchumi na utamaduni, kuhimiza mawasiliano kati ya mashirika ya utungaji wa sheria, kulinda utaratibu wa ushirikiano wa pande nyingi, na kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha