Maofisa wa UNESCO watoa wito wa ujumuishi wa AI katika mitaala ya shule barani Afrika

(CRI Online) April 24, 2025

Maofisa kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wametoa wito wa kujumuishwa kwa mitaala inayohusiana na Akili Mnemba (AI) katika shule za msingi na sekondari ili kuleta mageuzi katika mfumo wa elimu barani Afrika.

Akizungumza katika ufunguzi wa Wiki ya Kidijitali ya Ethiopia mwaka 2025 na Mkutano wa Kilele wa Elimu ulioandaliwa na kampuni ya Huawei, Mkurugenzi wa Ofisi ya Ushirikiano katika Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA), Rita Bissoonauth amesema, maendeleo ya AI barani Afrika yatasaidia kuboresha mfumo wa ikolojia wa uvumbuzi na endelevu kupitia kuendeleza suluhu za kidijitali.

Naye msomi mwandamizi katika Ofisi ya Ushirikiano ya UNESCO katika Umoja wa Afrika, Abdoulaye Salifou amesisitiza haja ya kuboresha fursa zinazotokana na AI na kuwezesha nguvukazi na teknolojia ya kidijitali ya Afrika ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika bara hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha