Wataalamu na watunga sera watoa wito wa michangamano zaidi ya kibiashara barani Afrika

(CRI Online) April 24, 2025

Wataalamu na watunga sera wametoa wito wa kufikia michangamano mikubwa ya kibiashara kati ya nchi za Afrika kupitia utekelezaji fanisi wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) na kuondoa vizuizi vya biashara ili kuhimili na kukabiliana na changamoto zinazotokana na hali isiyo na uhakika kimataifa na kuvurugika kwa biashara ya kimataifa.

Wito huo umetolewa kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kikanda kuhusu kuboresha maeneo ya kanda maalum za kiuchumi (SEZs), ambao umeandaliwa na Sekretarieti ya AfCFTA na kufanyika katika mji mkuu wa Djibouti, Djibouti City.

Akizungumza kwenye mkutano huo katibu mkuu wa AfCFTA Wamkele Mene amesisitiza kuwa, wakati dunia inakabiliwa na changamoto na kuvurugika kwa biashara kutokana Marekani kuongeza ushuru, Bara la Afrika linapaswa kubadili changamoto hizo kuwa fursa kwa kutumia vizuri hali ya sasa ya kimataifa na kuendeleza mfumo imara zaidi wa michangamano ya biashara kati ya nchi za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha