

Lugha Nyingine
Maonyesho ya 137 ya Canton yavutia wanunuzi zaidi ya 220,000 kutoka nchi za nje
Mnunuzi wa ng'ambo akitembelea eneo la vyombo vya kaure la Maonyesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, Aprili 23, 2025. (Xinhua/Deng Hua)
GUANGZHOU - Jumla ya wanunuzi 224,372 kutoka nchi na maeneo 219 walikuwa wameshiriki kwenye Maonyesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China, ambayo pia yanajulikana kwa jina la Maonyesho ya Canton, hadi kufikia hitimisho la kipindi chake cha pili jana Jumapili, Kituo cha Biashara ya Nje cha China kimeeleza.
Kipindi cha pili cha maonyesho hayo, inayojikita katika vyombo vya nyumbani vyenye sifa bora, ilianza Jumatano wiki iliyopita ikiwa na eneo la maonyesho lenye ukubwa wa mita za mraba jumla ya 515,000. Yanajumuisha vibanda 24,735 na waonyeshaji bidhaa 10,313, ikiwa ni ongezeko la 273 kuliko maonyesho yaliyopita.
Waonyeshaji zaidi ya 2,400 katika kipindi hiki cha maonyesho wanatambuliwa kama kampuni za teknolojia ya hali ya juu za kiwango cha kitaifa, kampuni ndogo "zenye uwezo mkubwa", au mabingwa wa kitaifa wa sekta ya viwanda vya utengenezaji bidhaa, ikiwa ni ongezeko la kampuni 100 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Maonyesho hayo yaliyopangwa kufanyika katika mji wa kisasa wa kusini mwa China wa Guangzhou kuanzia Aprili 15 hadi Mei 5, yameandaliwa katika vipindi vitatu vyenye mada tofauti. Cha kwanza kilijikita katika bidhaa za teknolojia ya hali ya juu, cha pili kinajikita katika vifaa bora vya nyumbani, na cha tatu katika bidhaa zinazoboresha maisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma