Uganda yatangaza mwisho wa mlipuko wa Ebola

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 28, 2025

Mwanamke akitembea kulipita bango kwenye hafla ya kutangaza kumalizika kwa Ugonjwa wa Virusi vya Ebola Sudan (SVD) mjini Mbale, Uganda, Aprili 26, 2025. (Picha na Patrick Onen/Xinhua)

Mwanamke akitembea kulipita bango kwenye hafla ya kutangaza kumalizika kwa Ugonjwa wa Virusi vya Ebola Sudan (SVD) mjini Mbale, Uganda, Aprili 26, 2025. (Picha na Patrick Onen/Xinhua)

MBALE, Uganda - Uganda imetangaza mwisho wa Ugonjwa wa Virusi vya Ebola vya Sudan (SVD) baada ya kukamilisha kuhesabu siku 42 za lazima za bila kuripoti maambukizi yoyote mapya yaliyothibitishwa, chini ya miezi mitatu baada ya virusi hivyo kugunduliwa katika mji mkuu, Kampala.

Waziri wa Afya wa Uganda Ruth Aceng ametangaza habari hiyo juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Michezo wa Shule ya Msingi ya Busamagga katika mji wa mashariki wa Mbale, moja ya maeneo yaliyoathiriwa na Ebola.

Miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inataka nchi itangazwe kuwa haina Ebola, ni lazima kufikia hali ambayo katika siku 42 (mizunguko miwili ya siku 21 za kuzaliana virusi) kutokuwa na maambukizi yoyote mapya kuripotiwa.

"Baada ya kukamilisha mizunguko miwili kamili ya kuzaliana virusi -- yaani, siku 42 -- tangu mtu wa mwisho aliyethibitishwa kuambukizwa kuruhusiwa kutoka hospitalini na bila kurekodi maambukizi mapya huku kukiwa na juhudi za kufuatilia siku zote, sasa natangaza rasmi mlipuko wa sasa wa Ugonjwa wa Ebola umekwisha nchini Uganda. Uganda sasa haina maambukizi ya Ebola," Aceng amesema.

Uganda ilitangaza mlipuko wa SVD Januari 30 baada ya muuguzi mwenye umri wa miaka 32 kufariki kutokana na ugonjwa huo katika Hospitali ya Rufaa ya kitaifa ya Mulago mjini Kampala.

Wakati wa mlipuko huo, wagonjwa 14, 12 wakiwa walithibitishwa kupitia vipimo vya maabara na wawili walioshukiwa kuwa wameambukizwa waliripotiwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Vifo vya watu wanne, wawili waliothibitishwa na wawili wanaoshukiwa, vilitokea, mamlaka ya afya ya nchi hiyo imeeleza. Jumla ya watu 10 walipona kutoka kwenye maambukizi hayo, na watu wengine 534 walitambuliwa kama waliokutana kwa karibu na watu walioambukizwa na wanaoshukiwa kuwa wameambukizwa.

Katika taarifa ya WHO, Chikwe Ihekweazu, kaimu mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, amesema uzoefu wa Uganda katika kudhibiti milipuko uliwezesha mwitikio wa haraka wenye ufanisi, na ulioratibiwa vizuri katika kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo.

"Mlipuko huu ulitupa changamoto kwa njia mpya. Uligusa jamii za mijini na vijijini kote nchini na ulitokea katika hali yenye ufinyu mkubwa wa mitaji kote duniani," Ihekweazu amesema.

Hakuna matibabu au chanjo zilizoidhinishwa za aina ya Ebola ya virusi vya Sudan, lakini kufanya mapema kwa huduma za utunzaji wa wagonjwa kumeonyeshwa kuwa kunaweza kupunguza vifo vya wagonjwa kwa kiasi kikubwa, WHO imeeleza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha