Waziri Mkuu wa Somalia afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri

(CRI Online) April 28, 2025

Shirika la Habari la Somalia limeripoti kuwa Waziri Mkuu wa Somalia Bw. Hamza Abdi Barre amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri jana Jumapili, akiwabadilisha waziri wa ulinzi, waziri wa mambo ya nje na naibu wa pili wa waziri mkuu.

Bw. Barre amemteua Bw. Ahmed Moallim Fiqi, waziri wa sasa wa mambo ya nje kuwa waziri ya ulinzi, huku akimteua naibu wa pili wa waziri mkuu Bw. Abdisalan Abdi Ali Dhaay, kuwa waziri mpya wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

Bw. Jibril Abdirashid Haji Abdi, aliyekuwa waziri wa ulinzi kwa wiki tatu tu, ameteuliwa kuwa naibu wa pili wa waziri mkuu. Kabla ya jukumu hilo, Bw. Jibril alikuwa waziri wa biashara na viwanda.

Bw. Fiqi, waziri mpya wa ulinzi, hapo awali aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani kwa miaka miwili na waziri wa mambo ya nje kwa mwaka mmoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha