

Lugha Nyingine
Msumbiji yapanga kutumia vizuri AfCFTA kustawisha biashara ya kikanda
Waziri Mkuu wa Msumbiji Bibi Benvinda Levi amezindua rasmi ushiriki wa nchi hiyo katika Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA).
Kwenye hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika siku ya Jumamosi, mwishoni mwa wiki kweye mji wa bandari wa Beira, Bibi Levi huku huku akibaisha thamani ya biashara kati ya nchi hiyo na nchi nyingine za Afrika imefikia dola za kimarekani bilioni 7.1 katika miaka mitano iliyopita, ametoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika viwanda na miundombinu chini ya mpango wa serikali wa “Msumbiji ya Viwanda”.
Waziri mkuu huyo pia amebainisha kuwa AfCFTA imeleta jukwaa kwa ajili ya kujenga uhusiano wa washirika wa kimkakati na kuhimiza shughuli za biashara na kiuchumi kwa sekta binafsi.
“Soko hili, zaidi ya kuharakisha ujenzi wa mfumo jumuishi wa mazungumzo kati ya sekta za umma na binafsi barani Afrika, pia lina uwezekano mkubwa wa kuongeza biashara ya Msumbiji na sehemu nyingine za bara la Afrika” amebainisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma