Wanamgambo wa RSF waua raia 31 mjini Omdurman nchini Sudan

(CRI Online) April 28, 2025

Makundi ya watu wa kujitolea nchini Sudan yamesema raia takriban 31 wameuawa na wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) huko Omdurman kaskazini mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan, ambao ni kikundi cha kujitolea, umesema kwenye taarifa yake kuwa kikosi cha RSF kimefanya mauaji hayo ya kutisha ya watu wenyeji 31, wakiwemo watoto wadogo kutoka eneo la Al-Salha katika mauaji ya halaiki yaliyoripotiwa katika eneo hilo.

Kamati Kuu ya Upinzani ya Al-Salha, kikundi kingine cha kujitolea, pia imeripoti mauaji hayo na kusema wapiganaji hao waliteka nyara raia wenyeji wasio na silaha na kuwaua.

Baadhi ya video zilizotolewa zinaonesha wapiganaji waliovalia sare za wanamgambo wa RSF na kuonyesha watu wanaoshikiliwa wakiwa wamekaa chini kabla ya kupigwa risasi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha