Malawi yaitaka Marekani itoe maelezo kuhusu kukataliwa kwa maombi ya visa ya maofisa wake

(CRI Online) April 28, 2025

Serikali ya Malawi imeiandikia Marekani kuhusu kiwango cha juu cha kukataliwa kwa maombi ya visa yaliyowasilishwa na maofisa wa serikali ya Malawi waliopanga kufanya safari za kikazi kwenda Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi imelalamikia tukio hilo katika barua ya mawasiliano iliyotumwa Aprili 23 kwa Ubalozi wa Marekani nchini Malawi, na kuvuja kwa umma Ijumaa ya wiki iliyopita.

Wizara hiyo imesema suala la visa linaamuliwa na serikali ya Marekani, na wizara imefanya juhudi kufuata itifaki mwafaka kwa mujibu wa hati ya kidiplomasia ya Mei 2, 2024.

Katika barua hiyo imeelezwa kuwa, wizara hiyo inaitaka serikali ya Marekani itoe maelezo kuhusu tukio hilo ingawa hadi sasa serikali ya Marekani haikuwa imetoa tamko lolote kuhusu suala hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha